Bifu kati ya wasanii wa Bongo Fleva, Ibraah na Harmonize, limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Ibraah kufunguka kuhusu tukio la zamani alilodai lilihusisha jaribio la unyanyasaji wa kingono kutoka kwa Harmonize.
RELATED; Ibraah Ft. Harmonize – Dharau
Katika ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ibraah alieleza kuwa wakati fulani alipokuwa na matatizo ya kifedha, alimuomba Harmonize msaada wa kulipia kodi ya nyumba. Badala ya msaada, alidai kuwa Harmonize alimuita chumbani kwake na kujaribu kumfanyia kitendo cha unyanyasaji wa kingono, ingawa jaribio hilo halikufanikiwa.
“Mimi siyo chakula bro, MIMI NI MSELA… naamini utabaki kuwa kaka,” aliandika Ibraah.
Mgogoro huu ulianza baada ya Ibraah kuonesha nia ya kuondoka kwenye lebo ya Konde Gang, inayomilikiwa na Harmonize. Alielezwa kuwa ili kuvunja mkataba wake, alitakiwa kulipa kiasi cha shilingi bilioni 1. Hii ilisababisha mvutano mkubwa kati yao.
Ibraah alikuwa msanii wa kwanza kusainiwa na lebo ya Konde Gang mwaka 2020. Alipata umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali, ikiwemo “Dharau” aliyomshirikisha Harmonize. Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, uhusiano wao umeonekana kuzorota kwa muda, na sasa umefikia hatua ya kutupiana maneno hadharani.
Bifu hili linaendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva. Wengi wanatarajia kuona jinsi hali itakavyokuwa katika siku zijazo na kama kutakuwa na suluhu kati ya wasanii hawa wawili.
Also, check more tracks from Harmonize;
This was beautiful Admin. Thank you for your reflections.