Haya hapa Matokeo ya Darasa la Nne 2025. Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza rasmi matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne (SFNA) pamoja na yale ya Kidato cha Pili (FTNA).
Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 10, 2026 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
👉 Matokeo ya Darasa la Nne yapo hapa
Njia Bora za Kuangalia Matokeo ya Darasa la Nne 2025/2026
Zifuatazo ni njia tatu (3) rasmi unazoweza kutumia kuangalia matokeo ya SFNA (Standard Four National Assessment):
1. Kuangalia Kupitia Tovuti Rasmi ya NECTA
Hii ndiyo njia inayopendekezwa zaidi kwa uhakika wa taarifa:
- Tembelea tovuti ya NECTA: www.necta.go.tz
- Bonyeza sehemu ya “Results”
- Chagua SFNA – Standard Four National Assessment
- Chagua mwaka 2025
- Tafuta mkoa, halmashauri, kisha shule yako
- Orodha ya wanafunzi pamoja na matokeo yao itaonekana
2. Kutumia Link za Moja kwa Moja (Direct Result Links)
Kutokana na msongamano mkubwa wa watumiaji kwenye tovuti ya NECTA, unaweza kutumia link mbadala:
- Matokeo ya Darasa la Nne 2025 – Link ya Moja kwa Moja
- NECTA Results Portal – SFNA
(Link hizi huwekwa mara tu matokeo yanapotangazwa rasmi)
3. Kuangalia Matokeo Kupitia SMS (Bila Intaneti)
Kwa wazazi au wanafunzi wasio na intaneti, NECTA hutoa huduma ya SMS:
- Fungua sehemu ya meseji kwenye simu yako
- Andika ujumbe kwa muundo huu:
NECTA NAMBAYAKOYA_MTIHANI MWAKA SFNA - Tuma kwenda 15700
Mfano:
NECTA PS0101-0001 2025 SFNA
