C - NEWS

Muigizaji Mkongwe Grace Mapunda (Tessa wa Huba) Afariki Dunia

Muigizaji Mkongwe Grace Mapunda (Tessa wa Huba) Afariki Dunia

Muigizaji maarufu wa filamu na tamthilia nchini Tanzania, Grace Mapunda, anayejulikana sana kwa jina la “Tessa” katika tamthilia Huba, amefariki dunia leo, Novemba 2, 2024. Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mtayarishaji wa tamthilia hiyo, @loulou_hassan.

RELATED: Nandy Ft Harmonize – Usemi Sina

Grace Mapunda, ambaye alikuwa mwigizaji mkongwe na mwenye ushawishi mkubwa katika sekta ya burudani ya Tanzania, alifariki dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Aziz Ahmed, muongozaji wa tamthilia hiyo na mshirika wake wa karibu kwa muda mrefu, alisema, “Ni kweli, amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamala.”

Ingawa hakuwa mgonjwa kwa muda mrefu, kwani alilazwa hospitalini siku mbili tu zilizopita, kifo chake ni pigo kubwa kwa wengi. Familia, marafiki na mashabiki wamekusanyika nyumbani kwake Sinza Vatican kumkumbuka na kutoa heshima zao.

RELATED: Remmy Ongala – Kifo Ft Super Matimilla

Muigizaji mwenzake, @idrissultan, pia amethibitisha taarifa za kifo chake na kuzungumzia mchango mkubwa alioutoa Grace katika sekta ya maigizo, akitambulika kama mama wa mastaa wengi kwenye filamu. Grace Mapunda atakumbukwa daima kwa mchango wake muhimu na nafasi yake katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Also, check more tracks from Alikiba;

Leave a Comment