ENTERTAINMENT

Mdundo Yazindua Kampeni ya Hip Hop @51 Mwezi wa Agosti

Mdundo Yazindua Kampeni ya Hip Hop @51 Mwezi wa Agosti

Mdundo.com ina furaha kubwa kutangaza kuanzishwa kwa kampeni yetu maalum ya Hip Hop@51, yenye lengo la kusherehekea na kuenzi muziki wa Hip Hop pamoja na wasanii wa nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Kenya, Tanzania, Uganda, Ghana, na Nigeria. Kampeni hii itakua ya mwezi huu wa Agosti.

Subscribe ili kupata DJ Mixes zaidi hapa Mdundo: https://mdundo.ws/CiMuzik

Kampeni hii inakusudia kuangazia safari ya muziki wa Hip Hop, kuanzia chimbuko lake hadi mabadiliko makubwa ambayo yamejiri ndani ya kipindi cha miaka 51. Tutatambua na kuenzi mchango mkubwa wa wasanii wetu kama vile Kutoka Kenya Wasanii kutoka Zoza Nation, Wangeci, Wakadinali, Catapilar, Gody Tenor, Nyanshinski, King Kaka, wa Tanzania ni kama vile Stamina, Gnako, Profesa Jay, Billnass ambao wameleta mapinduzi na kufanya muziki huu kuwa sehemu muhimu ya utamaduni wetu.

Tunawaalika wote kuungana nasi katika kusherehekea historia, hali ya sasa, na mustakabali wa muziki wa Hip Hop barani Afrika. Kutakuwa na shughuli mbalimbali za kuvutia, zikiwemo updates za mara kwa mara, mahojiano ya kipekee na wasanii, pamoja na matukio maalum yaliyoandaliwa kwa ajili ya mashabiki wa muziki huu.
Kaa ange kwa matangazo ya kusisimua, mahojiano ya kina, maandalizi ya dj mixes murua kwa jili yako shabiki wa mziki wa hip hop na matukio maalum ambayo yatabeba roho na hisia za muziki wa Hip Hop!

Leave a Comment