SPORTS

Matokeo ya Simba Vs Al Hilal Leo 31 Agosti 2024

Matokeo ya Simba Vs Al Hilal Leo 31 Agosti 2024

Simba SC iliwakaribisha Al-Hilal Omdurman kwenye uwanja wa KMC Complex leo, tarehe 31 Agosti 2024, majira ya saa 10 jioni kwa ajili ya mchezo wa kirafiki. Ingawa ni mechi ya kirafiki, ilitarajiwa kuwa na ushindani mkali kama sehemu ya maandalizi ya Simba kuelekea michuano ya kimataifa ya CAF.

RELATED: Matokeo Yanga Vs Kagera Sugar Leo 29 Agosti 2024

Simba SC imepanga kutumia mchezo huu kama kipimo muhimu cha maandalizi kabla ya kuanza kampeni yao ya Kombe la Shirikisho Afrika. Timu inatarajia kukutana na Al Ahly Tripoli ya Libya kwenye raundi ya kwanza. Kocha Mkuu, Fadlu Davids, alisisitiza umuhimu wa mchezo huu wa kirafiki kwa wachezaji, akisema kuwa utawasaidia kujiandaa kwa michezo ya kimataifa na kumwezesha kutathmini maendeleo ya timu kabla ya mchezo huo muhimu.

Katika maandalizi haya, Simba imefanya mazoezi makali na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki. Wakati huo huo, baadhi ya wachezaji wakiwa wameitwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya michezo ya kufuzu AFCON 2025, benchi la ufundi la Simba limekuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha kikosi kinabaki imara na tayari kwa mashindano yanayokuja.

Matokeo ya Simba Vs Al Hilal Leo 31 Agosti 2024
  • Simba SC 1 – 1 Al-Hilal Omdurman
    • Dakika ya 26: Ateba aliifungia Simba goli la kwanza.
    • Dakika ya 75: Serge Pokou alisawazisha kwa Al-Hilal.
    • 🏆 #Mechi ya Kirafiki
    • ⚽️ Simba SC 🆚 Al-Hilal Omdurman
    • 📆 31.08.2024
    • 🏟 KMC Complex
    • 🕖 4:00 PM

Leave a Comment