SPORTS

Matokeo Yanga SC vs Azam FC Leo 2 Novemba 2024

Matokeo Yanga SC vs Azam FC Leo 2 Novemba 2024

Mechi inayosubiriwa kwa hamu kati ya Young Africans SC (Yanga) na Azam FC inatarajiwa kuchezwa leo, tarehe 2 Novemba 2024, saa 12 jioni, katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Yanga SC wanajiandaa kwa ushindani mkali, wakiwa na morali ya juu baada ya ushindi wao wa hivi karibuni wa 1-0 dhidi ya Singida BS katika mechi yao ya 13, iliyochezwa mnamo tarehe 30 Oktoba 2024.

RELATED: Harmonize – Yanga Bingwa

Yanga SC pia walipata ushindi muhimu dhidi ya Coastal Union mnamo tarehe 26 Oktoba 2024 kwa bao 1-0, ambao uliwapa pointi muhimu na kuimarisha ari ya timu. Kwa sasa, Yanga wanajivunia rekodi nzuri ya kutopoteza michezo 20 mfululizo, huku wakishinda michezo 12 bila kuruhusu bao katika mechi 10 zilizopita.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa kwenye fainali ya Ngao ya Jamii, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Azam FC. Ingawa Azam ndio walitangulia kupata goli kupitia mchezaji wao wa zamani Feisal, Yanga walijibu kwa nguvu na kusimamia ushindi huo wa kihistoria.

Mashabiki wanaweza kutarajia mchezo wa kusisimua leo, huku Yanga wakilenga kuendeleza rekodi yao ya ushindi na Azam FC wakitafuta kulipiza kisasi kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Matokeo Yanga SC vs Azam FC Leo 2 Novemba 2024

Also, check more tracks from Marioo;

Leave a Comment