ILE siku ndio leo. Kilele cha wiki ya Simba kitafanyika, ambapo Wanasimba zaidi ya 60,000 watakutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kukamilisha vaibu lao la kuukaribisha msimu mpya chini ya kauli mbiu ya Ubaya Ubwela.
RELATED: Simba Day 2024 – Nyimbo 10 Bora Kwa Ajili ya Simba Day (Ubaya Ubwela)
Ndio siku ya furaha zaidi kwa Wanasimba. Saa chache zijazo wanakwenda kushuhudia furaha mpya baada ya kupitia miezi kadhaa ya machungu na karaha za kutoona ladha ya pira biriani waliyoizowea.