ENTERTAINMENT

S2kizzy – Baada ya P Funk Hakuna Producer Zaidi Yangu

S2kizzy - Baada ya P Funk Hakuna Producer Zaidi Yangu

Mtayarishaji maarufu wa rekodi nchini Tanzania, Salmin Kasimu Maengo, anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii S2KIZZY, ni mtunzi na mtayarishaji wa nyimbo. Anafahamika sana kwa kutayarisha nyimbo za Bongo Flava kama “Amaboko” ya Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz, na “Tetema” pia ya Rayvanny akimshirikisha Diamond Platnumz. Amesema kwamba baada ya kumpiku P Funk, yeye ndiye mtayarishaji bora zaidi wa muda wote nchini Tanzania.

RELATED: Marioo – Hakuna Matata (Prod. S2kizzy)

Akizungumza kwenye kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, S2kizzy alieleza kuwa Tanzania ina watayarishaji wengine wazuri ambao wamefanya kazi nzuri na kufikia mafanikio makubwa, kama vile Nahreel, T Touch n.k. “Baada ya P Funk Majani, ni mimi,” alisema S2kizzy, akiongeza kuwa hakuna mtayarishaji mwingine aliyewahi kutengeneza nyimbo hit 50, yeye ndiye aliyeweza kujitambulisha vyema zaidi ukimtoa P Funk, na katika orodha ya watayarishaji watatu bora zaidi Afrika Mashariki, lazima jina lake liwepo.

S2kizzy pia anamiliki magari ya kifahari, ikiwa ni pamoja na Range Rover na Mercedes-Benz, na amefanya kazi na wasanii wakubwa duniani. Ni mtayarishaji ambaye amefanikiwa kuibua vipaji vya watayarishaji wengine wengi, kama Trone n.k.

Alisisitiza kuwa ameweza kubaki kileleni kwa zaidi ya miaka minne, akitoka wimbo hit moja baada ya nyingine, na kusema kwamba bado yuko sana kwenye gemu, hatoondoka wala kuporomoka.

Leave a Comment