ENTERTAINMENT

Salim Kikeke Atambulishwa Rasmi kujiunga na Crown Media

Salim Kikeke Atambulishwa Rasmi kujiunga na Crown Media

Mwanahabari mashuhuri, Salim Kikeke, aliyewahi kuwa mtangazaji wa BBC Swahili, ametangazwa rasmi kuwa mmoja wa wafanyakazi wa Crown Media, chombo kipya cha habari kilichoanzishwa hivi karibuni na msanii maarufu wa Tanzania na Afrika Mashariki, Ali Kiba. Tangazo hilo limetolewa leo Jumatatu, tarehe 29 Aprili 2024.

RELATED: Mpiga Picha wa Millard Ayo, Zuchy Afariki Katika Ajali

Kikeke, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alielezea hisia zake kuhusu kujiunga na Crown Media, akisema, “Kwa heshima kubwa na taadhima, nachukua nafasi hii kutangazia umma kujiunga rasmi na familia ya Ufalme. Huu ni ushirikiano wa kipekee ambao unajumuisha majina makubwa katika sekta za sanaa na habari. Tunaunganisha nguvu kusonga mbele pamoja katika tasnia zetu. Hii ni hatua ya mwanzo katika safari ndefu na ya kusisimua ya kuleta mageuzi katika sekta ya habari na muziki. Nimerudi nyumbani, Tanzania, mahususi kwa ajili ya mradi huu. Karibuni sana nyumbani. Karibuni wote katika Ufalme.”

Crown Media, chini ya uongozi wa Alikiba, inalenga kuchanganya vipaji vya sanaa na habari ili kuleta mabadiliko na ubunifu katika tasnia hizi nchini Tanzania.

Leave a Comment