ENTERTAINMENT

Harmonize Adai Mungu ni Mwanamke Baada ya Miaka 30 ya Tafakuri

Harmonize Adai Mungu ni Mwanamke Baada ya Miaka 30 ya Tafakuri

Harmonize, jina la kisanii la Rajab Abdul Kahali, msanii maarufu wa Bongo Flava na mjasiriamali kutoka Tanzania, ameibua mjadala mkali kwenye mitandao baada ya kutangaza kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba anaamini Mungu ni mwanamke. Kauli hii imekuja baada ya miaka 30 ya maisha yake, ambapo amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi mashuhuri wa Afrika kama Burna Boy, Yemi Alade, Ruger, Sarkodie, na Naira Marley.

RELATED: Ibraah Ft. Harmonize – Dharau

Katika chapisho lake, Harmonize aliandika:

“WOW! Imenichukua miaka 30 kugundua ya kwamba pengine Mungu ni Mwanamke kwa asilimia kubwa! Nipo sambamba kabisa na vitabu vya dini visemavyo hakika Yeye hafanani wala hafananishwi! Lakini pia, pande zote kubwa mbili tunamuita Mungu BABA, kwa nini? Achilia mbali majukumu mengi zaidi anayoyafanya mwanamke katika familia kuliko mwanaume!!!

Tizama tu upatikanaji au hatua za mwanadamu utagundua mwanamke ndio CHANZO KIKUU; sote tumekamilika hatua kwa hatua tumboni mwa mwanamke! SUBHANALLAH! Mpaka wanyama na kila kiumbe! Haiwezi kuwa ni upendeleo, kama sio hivyo nifikiriavyo basi tukubaliane kuwa mwanamke ni MTU NA NUSU!!! Kuanzia leo hii, sijilinganishi wala kujiona bora zaidi ya MWANAMKE yeyote duniani. A WOMAN IS HUMAN AND HALF.”

RELATED: Marioo na Paula Kajala Watangaza Ujio wa Mtoto Wao

Maneno haya yamepokelewa kwa hisia mchanganyiko kutoka kwa mashabiki wake; baadhi yao wamekerwa, wakidai kwamba huenda mapenzi mapya yanamchanganya, huku wengine wakibashiri kwamba matumizi ya bangi yanaweza kuwa yamemvuruga. Hata hivyo, kauli ya Harmonize inaonekana kama jaribio la kutafakari kwa kina kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii na imani za kidini.

Leave a Comment