ENTERTAINMENT

Diamond asikitika Ziiki kuzuia wimbo wa Lava Lava ‘Kibango’

Diamond asikitika Ziiki kuzuia wimbo wa Lava Lava 'Kibango'

Diamond Platnumz, nyota wa muziki wa kimataifa na mmiliki wa lebo ya rekodi ya WCB Wasafi, ameeleza kusikitishwa kwake na kampuni ya usambazaji muziki ya Ziiki Media. Anadai kuwa Ziiki inazuia kuachiliwa kwa wimbo mpya wa msanii Lava Lava, ambaye amesainiwa chini ya lebo yake. Lava Lava, ambaye jina lake halisi ni Abdul Juma Idd, alizaliwa tarehe 27 Machi 1993 nchini Tanzania na anafahamika zaidi kwa wimbo wake maarufu “Tuachane.”

RELATED: Marioo na Paula Wanatarajia Mtoto wa Kike, Waandaa Baby Shower

Kupitia mitandao ya kijamii, Diamond Platnumz ameeleza masikitiko yake kwa kuchapisha ujumbe unaosema, “Inasikitisha kuona Ziiki Media inazuia kuachiliwa kwa wimbo wa Lava Lava ‘Kibango‘ leo na badala yake kushinikiza uachiliwe siku wanayoitaka wao, mwezi ujao bila sababu za msingi.”

Licha ya vikwazo, Diamond amewahakikishia mashabiki kuwa wimbo utatolewa leo hii, hata kama itabidi usambazwe kupitia njia mbadala kama WhatsApp. Amesisitiza umuhimu wa kuungwa mkono na mashabiki ili kupinga mbinu anazoona kuwa za udanganyifu kutoka Ziiki Media.

RELATED: Ujio wa Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz Ulivyowasisimua Wana Pangani

“Mashabiki msijali. #Kibango ya Lava Lava x Diamond Platnumz itatoka leo. Hata kama itabidi tusambaze kupitia WhatsApp, tunahitaji usaidizi wenu kikamilifu kuonyesha kuwa mashabiki wanataka muziki, sio propaganda. Acha muziki uachiliwe!” aliandika kwa hisia kali.

Diamond pia amefichua madai mazito zaidi dhidi ya Ziiki Media. Anasema tangu kukataa ofa ya Ziiki kununua hisa katika Wasafi Records na kuamua kuanzisha lebo yao, Ziiki imekuwa ikijaribu mara kwa mara kuvuruga kuachiliwa kwa nyimbo kutoka lebo ya Wasafi—kutoka kwa Diamond mwenyewe hadi wasanii wengine walio chini ya lebo hiyo. Ameeleza kuwa Ziiki imejaribu mbinu mbalimbali za kuiangamiza lebo na wasanii wake kisanii, lakini hawajafanikiwa kutokana na neema ya Mungu, talanta ya wasanii, na nguvu ya mashabiki.

“Ziiki wamekuwa wakijaribu kuvuruga utoaji wa nyimbo zetu mara kwa mara. Lakini niwakumbushe Ziiki kwamba Wasafi Records haikufika hapa ilipo kwa sababu tu ya vipaji vya wasanii pekee; ni kwa sababu ya neema ya Mungu, upendo, na usaidizi mkubwa tunao pata kutoka kwa watu. Leo, tutawaonyesha kwamba mashabiki wetu wana nguvu za kweli. Tutachia wimbo kwenye majukwaa yote, kisha tazameni jinsi mashabiki wetu wanavyoufanya wimbo huu kuwa mkubwa bila ya kuwepo kwenye majukwaa yoyote. Tazameni mitandao, vilabu, na hafla mbalimbali. Tutawaonyesha nguvu halisi ya mashabiki wetu!” Diamond alimalizia.

RELATED: Baba Levo Adai Kupigwa na Mkewe, Picha za Majeraha Zasambaa Mtandaoni

Wasafi Records, kupitia uongozi wa Diamond, inakumbusha Ziiki kwamba wana taaluma na uzoefu wa kutosha katika tasnia, wanafahamu taratibu sahihi na mikakati ya masoko kwa kuachia nyimbo. Wanasistiza kwamba wao ni wafaidika, sio waathirika, kila mara wimbo unapotolewa chini ya mipango yao makini, licha ya vikwazo vingi vinavyowekwa na Ziiki njiani.

Leave a Comment