MDUNDO DJ MIXES

Jay Melody Atuliza Joto La Subira Kwa Kuachia Video Ya “Baridi”

Jay Melody Atuliza Joto La Subira Kwa Kuachia Video Ya "Baridi"

Msanii nguli kutoka Tanzania, Jay Melody hivi karibuni amekata kiu ya mashabiki zake baada ya kuachia video ya “Baridi” ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu. 

RELATED: Mixes Tano Kali za Kupakua Wiki Hii Ndani Ya Mdundo.com

Subscribe ili kupata mixes mpya kila siku: https://mdundo.ws/CiMuzik

Video ya “Baridi” inakuja takriban miezi miwili tangu Jay Melody aachie ngoma hiyo ambayo kupitia mtandao wa YouTube, kufika sasa imeshasikilizwa mara Milioni 2.4 huku pia ikiwa imetumika kusindikiza video ya Miss World siku chache zilizopita. 

Kwenye video, Jay Melody anaonekana akiwa anafurahi na mpenzi wake kwenye maeneo tofauti tofauti ikiwa imepambwa na hadithi nzuri ambayo inaendana na mashahiri, mahadhi na maudhui ya ngoma nzima. 

Kelly Film ndiye amehusika katika kutayarisha video hii ambayo kufika sasa Inaonekana kuvutia mashabiki wengi. 

Leave a Comment