ENTERTAINMENT

Wema Sepetu amburuza mahakamani Aristostle

Wema Sepetu amburuza mahakamani Aristostle

Mwanahabari na mwandani wa Irene Uwoya , Aristostle yupo katika wakati mgumu baada ya kuzungumza maneno kuhusu muigizaji maruufu nchini Tanzania Wema Sepetu, ambayo yalichukuliwa kama udhalilishaji wa jinsia ya kike kwa ujumla.

RELATED: Zuchu atavishwa pete siku ya Valentines – Mama Dangote athibitisha

Wema Sepetu amemfikisha Aristostle mahakamani baada ya kushauriana na wakili wake kuhusu matamshi ya mwanahabari huyo.

Kupitia kituo kimoja cha radio nchini humo, wakili wa Wema Sepetu ameeleza kwamba wameenda makamani kuhakikisha mwigizaji huyo amepata kulipwa kutokana na maneno ya udhalilishaji yaliyotolewa na Aristostle.

Ikumbukwe Aristostle alionyesha kujuta maneno yake na akajitokeza kumuomba msamaha muigizaji huyo. Msamaha wa mwanahabari huyo unaonekana kugonga ukuta, huku mwanasheria wa Wema akiwa ashamfungulia kesi mwanahabari huyo.

“Tunafuatilia kuona kwamba msanii wangu amepata kulipwa. kwa sababu ametukanwa, na watu walio na pesa, Irene ana pesa natumai atamsimamia Aristotle na yeye amlipe mteja wangu. Msamaha aliyeomba Aristotle hufai kamwe kuitwa msamaha kwa sababu alijua vyema alichokuwa akitenda,” alisema mwanasheria wa Wema Sepetu.

RELATED: Marafiki zangu ni Wanaume, Wanawake ni wanafiki – Irene Uwoya

Kutokana na cheche za maneno na matusi ya mashabiki yaliyotawala ukurusu wa Aristostle imemlazimu kuchokonoa ukurusa wake wa instagram.

Ni kweli wazi kuwa chochote usemacho kuhusu mtu mwingine kufikiria kabla ya kutenda usije ukajichimbia kaburi yako mwenyewe.

Also, check more tracks from Zuchu;

Leave a Comment