ENTERTAINMENT

Mbosso kuachia Albamu mpya mwaka huu 2022

Mbosso kuachia Albamu mpya mwaka huu 2022

Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuf Kilungi maarufu kama Mbosso Khani amezidi kunogesha kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kutangaza kuwa ataachia albamu mpya mwaka huu.

RELATED: Mbosso Ft Zuchu – For your Love (Prod. Mocco)

Staa huyo ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Nigeria, amesema kuwa kwa sasa ana kazi nyingi sana ambazo amekwisha-ziandaa hivyo mashabiki zake wategemee yeye kuachia albamu au hata EP kwa mwaka wa 2022.

“Mwaka huu pia natarajia kutoa album lakini kama haitakuwa album basi itakuwa EP kwa sababu kazi zipo nyingi sana za sehemu tofauti tofauti. Tuna collabo na nchi tofauti tofauti. Namshukuru Mungu huu ni moja ya mwaka ambao watu watasikia sound ya tofauti sana kutoka kwangu,” alizungumza Mbosso.

Iwapo Mbosso atatimiza ahadi yake ya kuachia albamu, basi albamu hiyo inatarajiwa kuwa ya pili kwa Mbosso baada ya ‘Definition of Love’ ya mwaka 2021 kuweza kufanya vizuri sana.

Aidha, Mbosso alitumia fursa ya mahojiano hayo kueleza kuwa kipindi yupo nchini Nigeria amefanya collabo nyingi sana na wasanii wa nchi hiyo na hivyo mashabiki wategemee vitu vizuri.

RELATED: Mbosso Ft Diamond Platnumz – Karibu (Prod. Abbah)

“Safari ilikuwa ina manufaa makubwa sana kwa sababu mara ya mwisho kwenda Nigeria ilikuwa 2019 nilienda kwa ajili ya tuzo za Afrimma nikarudi. Safari hii nilienda kwa ajili ya kujizatiti na kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti kuandaa kazi zangu mimi ukiachilia mbali hizo collabo,” alizungumza Mbosso.

Also, check more tracks from Mbosso;

Leave a Comment