Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) usiku wa kuamkia leo walitoa tuzo za msimu wa 2020/21 kwa wachezaji, makocha, waamuzi na viongozi ambao walifanya vizuri. Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta, Jijini Dar es salaam.
Tuzo hizo ziligawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni ligi kuu, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) maarufu kama FA na Ligi ya Wanawake.
Orodha ya washindi wa tuzo za TFF 2021 – Tazama hapa
- Mfungaji bora kombe la Shirikisho (ASFC) – Reliants Lusajo (Namungo).
- Mfungaji bora Ligi ya Wanawake – Aisha Masaka (Yanga).
- Mfungaji bora Ligi Kuu Bara – John Bocco (Simba).
- Timu yenye nidhamu katika ligi ya Wanawake – Ruvuma Queens.
- Timu yenye nidhamu katika Ligi Kuu Bara – Coastal Union (Tanga).
- Meneja bora wa Uwanja – John Nzwalla (Nelson Mandela Rukwa)
- Kamishna bora – Pili Mlima (Arusha).
- Mwamuzi bora msaidizi kwa wanawake – Sikuzani Nkurungwa (Njombe).
- Mwamuzi bora kwa Wanawake – Amina Kyando (Morogoro).
- Mwamuzi bora msaidizi ligi Kuu soka Tanzania Bara- Frank Komba.
- Kocha bora kwa wanawake ni – Edna Lema (Yanga Princes).
- Kocha bora ligi kuu bara – Didier Gomes (Simba).
- Mhamasishaji bora – Bongozozo.
- Mchezaji bora chipukizi Wanawake- Asha Juma (Alliance)
- Mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu Bara – Abdul Suleiman (Coastal Union).
- Kipa bora Azam Federation Sports – Aishi Manula (Simba).
- Kipa bora kwa Wanawake – Janeth Shija (Simba Queens).
- Kipa bora wa Ligi Kuu Bara – Aishi Manula (Simba).
- Beki bora wa Ligi Kuu Bara – Mohammed Hussein (Simba).
- Kiungo bora wa Ligi Kuu Bara – Clatous Chama (Simba).
