ENTERTAINMENT

Mambo 20 yanayoonyesha una ukichaa wa mapenzi

Mambo 20 yanayoonyesha una ukichaa wa mapenzi
 1. Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
 2. Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
 3. Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
 4. Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.
 5. Kusema wanawake wote sawa.
 6. Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.
 7. Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.
 8. Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!
 9. Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?
 10. Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!
 11. Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!
 12. Kumhonga mwanaume ili akuoe!
 13. Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!
 14. Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!
 15. Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!
 16. Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.
 17. Kumsomesha mtu ili uje umuoe!
 18. Kumng’ang’ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!
 19. Kuwaeleza mashosti zako ‘utam’ anaokupa mtu wako!
 20. Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..

Nimeipaste kama ilivyo kama imekugusa Nivumilie

RELATED: Sifa kuu 10 za mwanamke mwema (wife material)

Leave a Comment