ENTERTAINMENT

TUONGEE: Eti ni kweli hizi tabia 12 ndio zinawafanya wanawake wasiolewe?

TUONGEE: Eti ni kweli hizi tabia 12 ndio zinawafanya wanawake wasiolewe?

Habari mpendwa karibu tena kwenye tovuti yetu pendwa kabisa, Mada yetu ya leo ni Eti ni kweli hizi tabia 12 ndio zinawafanya wanawake wasiolewe?

Pitia pointi hizi kisha na wewe usisahau kuweka comment yako hapo chini au unaweza kubofya hapa ili ku-comment.

TUONGEE: Eti ni kweli hizi tabia 12 ndio zinawafanya wanawake wasiolewe?

1. Tamaa ya utajiri, fedha na mali nyingi pasipo kutambua kuwa vitu hutafutwa, hapa wengi hupoteza nyota zao kwa kukataa wengi wenye kipato cha kawaida na kujirahisisha kwa wenye nazo ambao kwa bahati mbaya wengi wao sio waoaji bali ni wahuni tu na watu wa anasa na kula bata mjini

RELATED: Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi

2. Dharau, maringo, kiburi na mashauzi yaani we kila mtu akikusogelea na kujaribu kuzungumza na wewe unaanza kumpandisha na kumshusha kisha una msonya. Wengi huishia kukupotezea wakijua either umewadharau au tayari una mtu wako ndio maana nyodo nyingi.

3. Huna Jumapili wala Ijumaa yaan huendi kanisani wala Msikitini husali wala humuombi Mungu hakika lazima wahuni watapata nafasi kwako na kukuchezea mpaka uchakae kama mtumba wa ilala boma.

MUNGU NI NGUZO KUU YA BARAKA ukimuomba hakika atakuepushia kuingia midomon mwa dubu na fisi wanaokuwa wakikuvizia na kuja kama MALAIKA. Atakupa ufahamu wa kuwatambua na kuwashtukia mapema.

4. Kuvaa nguo za ajabu ajabu kama changudoa. Sijui ni nani aliyewaambia kuwa mkivaa hivyo mnapendeza!

Unakuta binti unavaa kama mcheza show za Casino yaani ukipita nguo yaonyesha kila kitu ukiinama ndio balaa kabisa yaani kimin kinafunuka kila kitu nje nje kwa style hiyo nani atakupeleka kwao?

5. Kujipaka marangi ya ajabu ajabu usoni kama mwali wa kimakonde au kizaramo kwanza mnatutisha tu.

6. Kupenda kujirahisisha au kujipendekeza pendekeza kwa wanaume, yani ukiguswa kidogo tu twende.

7. Kuwa na picha karibia 500 Facebook, Twitter nk halafu picha zenyewe hazieleweki yani zimepigwa katika mavazi au mapozi ya ajabu ajabu, mara umebinua makalio, mara tumbo, mara mdomo, Haaaaa!

8. Kila unachofanya basi unakimbilia kupost mfano kwenye Facebook account
yako au Instagram na nyinginezo hata ukienda haja basi lazima upost.

9. Ni mtu wa maneno maneno yani we kila unachokiona unaongea na kuropoka ropoka tu hauna break! mwanamke gani?

10. Huna mawazo ya malengo endelevu yani we kwenye bichwa lako kumejaa umbea tu sijui leo Wema Sepetu amefanya nini? Sijui Kim, Lupita amefanya vile na upuuzi mwingine.

RELATED: Ukipata mwanamke mwenye sifa hizi 16 usimwache

11. Mizinga. Yani siku ya pili tu baada ya kukutongoza unaanza ” honey nataka galaxy” Htc” Huawei” mara baby nimeona nguo nzuri mara ooh baby yaani njaa inauma” , utasindikiza harusi za wenzio hadi upigwe alama..

12. Tabia nyingine ni kutowajibika na kupenda kukaa tuu na kupokea au kila kitu kusaidiwa. Mwishowe unakua mzigo sasa

3 Comments

  • Jamani Mwanamke lazma ujipambe na kupendeza, Pia kuvaa nguo fupi sio huuni bhana ni imani potofu tu, nguo fupi katika level gani?

  • Sababu hizo zote kweli kabisa zinachangia wanawake wengi kukosa kuolewa;lakini mimi binafsi naziona sababu mbili hapo kuwa ndizo zinazowakumba wanawake wengi zaidi.

    Kwanza ni hiyo ya kupenda kuolewa na wanaume ambao tayari wameshafanikiwa kiuchumi ili kupata sifa kuwa nimeolewa na mwanaume mwenye mawe lakini pia ni kutokuwa tayari kuanza chini mtu ndo anaanza anataka awe na gari la gharama kama mwenzake aliyeolewa miaka 15 iliyopita hapo ndipo tunapofeli wadada

    Lakini sababu nyingine kubwa ni kuwa rahisi kulala na kila mwanaume anayeanza naye mahusiano, hayajafika hata umbali wowote tayari, hiyo inawakumba wengi

    Binafsi hizo sababu mbili naona ndizo sababu zinazowakumba wanawake wengi zaidi kuliko hizo zingine ingawa nazo kwa baadhi ya wanawake zimechangia sana kutokuolewa ikiwemo kuongea sana kwa kuropoka, hakuna mwanaume anayependa tabia hiyo lakini hiyo ipo kwa baadhi tu ya wanawake

Leave a Comment