ENTERTAINMENT

Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko “Tunakuombea”

Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko
Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko: Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Harmonize ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe mzito unaomhusu Rich Mavoko.

Kumbuka kwamba Harmonize na Rich Mavoko waliwahi kufanya kazi pamoja na kwa ukaribu sana walipokuwa WCB chini ya Diamond Platnumz.

Kwa sababu tofauti tofauti wote waliamua kuondoka katika record label hiyo, akiazna Rich Mavoko kisha Konde Boy.

Kupitia account yake ya Instagram Harmonize aliandika ujumbe mzito kwa Rich Mavoko.

Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko

Familia Ngapi Zipo Nyuma Ya @richmavoko ..?? Na zinamtegemea Yeye KwaKila Jambo Hasa Hili La Kupata Mkate Wa Kilasiku VP Kuhusu Ndoto Za Familia Hizo Na Zinaishije Katikwa Wakati Huu…???

Ndoto Ngapi Za Wasani Ambao Wanategemea Kuzifikia Hizo Ndoto Kupitia Mavoco ..?? Na Nyuma Ya Hao Wasanii Kuna Familia NyenginePia ..??

Jeee Maumivu Malala Miko Ya Wazazi Wake Hasa Mama Mzazi Ambae Ndio Kama Roho Yake …!!!

Ushajiuliza Ni Kauli Ngapi Za Uchungu Anazitoa Ambazo Zinaweza Kumpata Kila Anaefurahishwa Na Hili Kwa Makusudi ..???

Mana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata …!!

La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anaefurahia Na Kuifanya Hii Kuwa Ni Habari Njema Kwake Ya Kumfanya Atembee Kifua Mbele Na Hata Kuandika Mtandaoni Kwa Furaha MAVOCO KAPOTEA muulize Anafaidika Nanini …???

Mungu Anasababu Na Maana Yake Bro @richimavoco Kama Mdogoako Nakuombea Najua Ukimya Wako Unamaana Kubwa Sanaa.

Ndani Yako Ninachojua Ni Kujiweka Sawa Na Kutuletea Kazi Zingine Tunakupenda Na Tunakuombea Mungu Akufanyie Wepesi…!!!

Let’s Go Bro Mdogoako Rafiki Yako Nipo Hapa Muda Wowote…!!!! RAMADAN KAREEM” – Huo ndio Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko

Ujumbe mzito wa Harmonize kwa Rich Mavoko

Leave a Comment