ENTERTAINMENT

Stamina afunguka kuhusu mdada mjamzito kwenye “Kaka Tuchati”

Stamina afunguka kuhusu mdada mjamzito kwenye "Kaka Tuchati"

Mmoja kati ya rapa maarufu nchini Tanzania na anayefanya poa kabisa kwenye game Stamina amefunguka kuhusu mdada mjamzito aliyekuwa anapita-pita chumbani kwenye video yao mpya Kaka Tuchati pamoja Roma Mkatolika.

RELATED: Rostam (Roma & Stamina) – Kaka Tuchati | mp3 Download

Kumbuka Stamina alipata shida ya ndoa, alifunguka na kuzungumza mengi kuhusiana na ndoa yake kwenye wimbo wake wa “Asiwaze” ambao ulitrend na kukaa kwenye chart mbalimbali za muziki Tanzania.

RELATED: Stamina Ft Atan – Asiwaze | mp3 Download

kipitia mtandao wa Instagram Stamina alisema:-

“TAARIFA YA FURAHA!! DADA anayeonekana kwenye VIDEO ya KAKA TUCHATI akiwa anapita kwenye verse ya tatu akiwa na MIMBA amejifungua MTOTO WA KIUME jioni hii…

Na kwa heshima anayotupa na ambayo ROSTAM tumempa ameamua MTOTO HUYO kumpa jina la ROSTAM kama kumbukumbu kwenye maisha yake, tunamtakia heri na baraka MAMA NA MDOGO WETU MPYA, BABA zake wadogo tutakua nae BEGA KWA BEGA….. Tunasubiri akue tuchati nae??? #rostam #kakatuchati” – Aliandika Stamina.

Bofya hapa kuitazama video ya Kaka Tuchati

Stamina afunguka kuhusu mdada mjamzito kwenye "Kaka Tuchati"
Stamina afunguka kuhusu mdada mjamzito kwenye “Kaka Tuchati”

Leave a Comment