Mfalme wa R&B tokea nchini marekani Usher, amejikuta katika wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Nicki Minaj (Barbz), baada ya mkali huyo kusema kwamba Minaj ni zao la Lil Kim.
Usher alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kumalizika battle kati ya Ludacris na Nelly, alipoulizwa kama ingekua vizuri Nick Minaj akishandanishwa na LIL KIM.
Usher alisema kwamba haitakua vyema kuwashindanisha, kwasababu Nick Minaj ni zao (product) ya LIL KIM, kauli ambayo iliwakera mashibiki wa Minaj na kuanza kumshambulia mitandaoni..
Source: WasafiTv Tanzania