Jozi za viatu za nguli wa mchezo wa kikapu Michael Jordan za kwanza kabisa na alizozivaa mwaka 1985 zimeweka rekodi ya kuuzwa kwa kiasi cha dola za Marekani 560,000 zaidi ya Tsh. Billioni 1.2 ( $ 560K ) kwenye mnada wa mtandaoni.
Jozi hiyo ya viatu ya Nike Air Jordan 1s, ilivaliwa na Jordan wakati wa msimu wake wa kwanza akiwa kinda na klabu ya Chicago Bulls.
Awali ilitarajiwa vigeuzwa kwa dau la kati ya dola 100,00 mpaka dola 150,000 kwenye kampuni ya mauzo ya Sotheby’s.
Kiatu cha kwanza cha AIR JORDAN chauzwa Sh. Billioni 1.3
Source: WasafiFm Tanzania