E NEWS

Diamond, Barna & more at Africa Day Benefit Concert at Home – 25 May 2020

READ IN ENGLISH | SOMA KWA KISWAHILI

Diamond Platnumz, Burna Boy, Angelique Kidjo, Nandy na wengine watatumbuiza siku ya Jumatatu (Mei 25) ijayo kwenye tamasha la “Africa Day Benefit Concert At Home”

Tamasha hilo lilioandaliwa na Kituo cha MTV Base pamoja na Youtube kwa lengo la kusherekea siku ya Afrika na kukusanya fedha kwaajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Corona litaongozwa na muigizaji maarufu wa Uingereza, Idris Elba.

Wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo ambalo litaoneshwa Live kwenye mitandao ya Kijamii ya MTV Base ni pamoja na Angelique Kidjo, Burna Boy, Diamond Platnumz, Sauti Sol, AKA, Yemi Alade, Sho Madjozi, Nandy, M.anifest, Tiwa Savage, Stonebwoy na wengine.

Mapato yote kutoka kwenye tamasha hilo yataelekea kwa mahitaji ya kiafya na ya lishe ya familia zilizoathiriwa zaidi na maambukizi ya COVID-19.

Diamond, Barna & more at Africa Day Benefit Concert at Home – 25 May
Spread the love

Leave a Comment