ENTERTAINMENT

Ninaweza kujikinga vipi na Virusi vya Corona?

Virusi vya Corona vinasambaa vipi?

Watu wanaweza kupata Virusi vya Corona kutoka kwa watu walioambukizwa.

Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. Iwapo mtu anagusa maji maji kama mafua, mate na makohozi ya mtu aliye na virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua anaweza kupata virusi vya Corona.

Ninaweza kujikinga vipi na Virusi vya Corona?

  1. Nawa vizuri na kila wakati mikono yako kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu kwa angalau sekunde 20.
  2. Kaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.
  3. Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi.
  4. Hakikisha wewe, na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya.
  5. Baki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri. Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kwa sababu huko wataalamu watakupatia msaada muhimu.
  6. Epuka kuwa sehemu yenye msongamano, kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye yenye mgandamizo wa hewa.
  7. Fuatilia taarifa za afya na matangazo yake kuhusu virusi vya Corona.

Source: DW

Leave a Comment