Haya ni mawazo yangu tu, mimi ni Chedaa, wadau msiniue! Tangu Mbosso alipoanza safari yake kama msanii wa Bongo Fleva wa kujitegemea, hakuna mwaka ambao jamaa huyu hajasitahili kushinda tuzo ya mwandishi bora. Jamaa anaandika ngoma zenye uzito wa balaa!
RELATED: D Voice Ft Mbosso – Tunapendana
Nimeona Marioo amechukua tuzo, na sisemi kwamba Marioo hajui kuandika – la hasha! Lakini ukimlinganisha na Mbosso, ni kama umbali wa mafanikio ya Career ya Zuchu na Anjella – mbali sana. Sio kwa ubaya, Marioo ni mbunifu sana na ana uwezo mkubwa, lakini linapokuja suala la uandishi, Mbosso ni baba yao.
Jay Melody naye yupo vizuri, na kwa maoni yangu, Mbosso ni noma zaidi! Sikiliza kazi yake hapa chini kisha niambie mawazo yako kwenye comments. Nini unadhani? 🙌
Also check more tracks from Mbosso;