Ni wakati mwingine wa kusherehekea vipaji vya wasanii wetu wa Tanzania kupitia Tanzania Music Awards 2024! Hii ni fursa ya kipekee kwako kumpigia kura msanii wako unayemkubali kwenye vipengele tofauti na kuwa sehemu ya mafanikio yao. Nyimbo zao maarufu tayari zinapatikana kwenye Mdundo.com, hivyo unaweza kuzisikiliza wakati ukijiandaa kupiga kura!
Hapa kuna orodha ya wasanii wenye nyimbo zinazopatikana kwenye Mdundo.com ambao wamepewa nafasi ya kushinda tuzo:
- Wimbo Bora wa Mwaka (Best Song of the Year) :
Wimbo gani umevibe nao sana mwaka huu? Hakikisha unapiga kura kwa wimbo unaoupenda zaidi.
- “Baridi” – Jay Melody
- “Mahaba” – Ali Kiba
- “Single Again” – Harmonize
- Msanii Bora wa Kike Bongo Flava (Female Bongo Flava Artist)
Nandy amejidhihirisha kuwa Gwiji wa kike wa Bongo Flava, je, unaona anaweza kuibuka mshindi? Piga kura kumsaidia kupata ushindi. - Msanii Bora wa Kiume Bongo Flava (Best Bongo Flava Artist – Male)
Kura yako inaweza kuwa kipimo cha ushindi kati ya hawa wakali wa Bongo Flava. Nani atashinda? Ni juu yako kuamua!
- “Sawa”- Jay Melody
- “Love Song” – Marioo
- “Mahaba” – Alikiba
- “Single Again” – Harmonize
- Msanii Bora wa Singeli (Best Singeli Artist)
Dulla Makabila anakuja kivingine na Singeli yake kali ya Nije ama Nisije. Usikose nafasi ya kumpigia kura! - Album Bora ya Mwaka (Best Album of the Year)
Hizi albamu zimeleta mabadiliko makubwa kwenye muziki wetu. Ni ipi imekugusa zaidi? Piga kura kwa albamu bora!
- “Most People Want This” – Navy Kenzo
- “Visit Bongo” – Harmonize
- “Swahili Kid” – D Voice
- Mwimbaji Bora wa Dansi (Best Dansi Artist)
Christian Bella ameendelea kuwa mfalme wa kusakata rumba! Una nafasi ya kumuwezesha kushinda. - Wimbo Bora wa Hip Hop (Best HipHop Song)
Nyimbo hizi zimewasha moto kwenye ulimwengu wa Hip Hop. Wimbo gani ni bora zaidi? Kura yako ni muhimu!
- “Stupid”- Young Lunya
- “Bobea” – Joh Makini
- “Machozi” – Stamina & Bushoke
- Msanii Bora wa Hip Hop (Best HipHop Artist)
Wasanii hawa wameweka historia kwenye Hip Hop ya Tanzania. Mpigie kura yule unayeamini ameonesha uwezo wa juu zaidi.
- Young Lunya
- Kontawa
- Joh Makini
- Rosa Ree
- Stamina
- Kolabo Bora (Best Collaboration)
Kolabo hizi zimeitikisa game ya muziki. Kina nani wameshirikiana vizuri zaidi? Kura yako itasema yote!
- “Sele” – Mbosso & Chley
- “Sumu” – Alikiba & Marioo
- “Enjoy” – Jux & Diamond Platnumz
- Msanii Bora wa Kike (Best Female Artist)
Malkia wa muziki, Nandy, anawania tuzo nyingine. Ni msanii anayestahili kupata heshima hii? - Msanii Bora wa Kiume (Best Male Artist)
Wasanii hawa wa kiume wameendelea kutamba na ngoma kali mwaka huu. Mpigie kura msanii wako bora!
- “Shisha” – Marioo
- “Single Again” – Harmonize
- “Nitasema” – Jay Melody
- “Sumu”- Alikiba
- Video Bora (Best Video)
Video hizi zimesisimua mashabiki na kushika nafasi kubwa kwenye mitandao ya kijamii. Ni ipi imekuvutia zaidi? Kura yako ni muhimu!
- “Maokoto” – Billnass
- “Single Again” – Harmonize
- Mtunzi Bora wa Nyimbo (Best Song Writer)
Maneno yana nguvu, na hawa ndio waandishi bora wa nyimbo mwaka huu. Ni nani unadhani ana uwezo wa kipekee?
- Mbosso
- Dulla Makabila
- Jay Melody
- Marioo
Jinsi ya Kupiga Kura
Kupiga kura ni rahisi sana! Unaweza kupiga kura kwa wasanii wako pendwa kwa kupitia tovuti rasmi ya Tanzania Music Awards(https://tanzaniamusicawards.com ) au kwa kutumia njia za ujumbe mfupi (SMS) kwa kufuata maelekezo yaliyoorodheshwa kwenye tovuti hiyo. Usikose nafasi hii adhimu ya kuwa sehemu ya mchakato wa kumpa ushindi msanii unayempenda.
Kumbuka, unaweza kujiburisha na Djmix mbali mbali https://bit.ly/DJmix-Bongofleva