ENTERTAINMENT

Rayvanny Amjibu Baddest Kuhusu Madai ya Wimbo ‘Sensema’

Rayvanny Amjibu Baddest Kuhusu Madai ya Wimbo 'Sensema'

Baddest 47 ametoa ushahidi wa mazungumzo ya DM na Rayvanny kuhusu kuachia wimbo wao wa pamoja “Sensema” mnamo Aprili 25 mwaka huu. Ameomba Chui azungumze ukweli kuhusu wimbo huo aliofanya na Harmonize badala yake.

RELATED: Rayvanny Ft Harmonize – Sensema 

Rayvanny amemjibu Baddest 47 kuhusu madai ya wimbo “Sensema“, akieleza kwamba walipanga kuufanya pamoja na S2kizzy lakini mawasiliano yalikwama. Ameongeza kuwa timu yake ilimtaarifu Baddest bila mafanikio na ameshangazwa na jinsi mambo yalivyo sasa. Aidha, amedai kwamba hata yeye hayupo kwenye wimbo “SIJI” wa Zuchu licha ya kuimba.

Staa huyo wa Bongo Fleva Rayvanny ameandika:

To my home Boy Baddest, unajua vile nakukubali na hatujawahi kuwa na tofauti hata mara moja. Speaking about “Sensema”, wewe unajua ukweli kuwa wimbo tuliandaa mimi na Zombie na tulitamani uwe sehemu ya wimbo huu!! Na ukatumiwa lakini nilisubiri mrejesho bila mafanikio, na sisi tukaendelea na project. By the time umemaliza sisi tuko na plans zingine kabisa.

Mbali na hapo, timu yangu walikupigia na wakakuambia nini kinaendelea. Nashangaa imekuaje hadi mambo yamefika huku. Pengine haikua riziki upande wako, lakini sisi watoto wa nyumbani tushafanya kazi na sio mwisho kufanya kazi zingine. Siji ya my sis Zuchu niliimba lakini kwenye wimbo sipo. Hiyo ni kawaida sana kwenye muziki. Kuna nafasi ya miziki mingine, we family.

Mtayarishaji wa muziki kutoka Pluto S2kizzy maarufu kama Zombie, amefafanua kuhusu wimbo anaodaiwa ku-copy kutoka kwa Baddest 47. Wimbo huo ameutoa kwa Rayvanny na Harmonize wa “Sensema“.

1 Comment

Leave a Comment