SPORTS

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC ‘Try Again’ Ajiuzulu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC 'Try Again' Ajiuzulu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Muhene, maarufu kama “Try Again,” ametangaza kujiuzulu kutoka nafasi yake leo, Juni 11, 2024.

RELATED: Diamond Platnumz – Komasava Ft Khalil Harrison X Chley (Prod. S2kizzy)

Hatua hii inafuatia siku chache baada ya wajumbe kadhaa wa bodi kujiuzulu, huku ikiripotiwa kuwa Try Again alikuwa amegoma kuachia madaraka. Katika tangazo lake, amemwomba mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji, kurejea na kuchukua nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo, huku yeye akibaki kuwa mwanachama wa kawaida.

Akizungumza kupitia televisheni, Try Again alisema: “Kwa maslahi mapana ya Simba na kwa kutambua mpira ni mchezo wa hisia, nimemwomba mwekezaji wetu Mohamed Dewji MO arejee kama Mwenyekiti wa Bodi nami nitasalia kama mwanachama na kiongozi ambaye nipo tayari wakati wowote kuitumikia Simba. Kwa maana hiyo, natangaza kuondoka kwenye kiti.”

Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi.

Also, check more tracks from Diamond Platnumz;

Leave a Comment