Muda mfupi baada ya mtayarishaji maarufu wa rekodi nchini Tanzania, Salmin Kasimu Maengo, maarufu kama S2KIZZY, kujinasibu kwamba hakuna mtayarishaji anayeweza kulinganishwa naye Afrika Mashariki na katika kizazi cha sasa, Sweetbert Charles Mwinula, anayejulikana kama Abbah Process (amezaliwa tarehe 28 Julai 1994), ambaye ni mwanamuziki na muandaaji wa muziki nchini Tanzania, alijitokeza na kudai kuwa amekuwa kimya kwa mwaka mzima bila kutayarisha ngoma yoyote, ila bado mitaa inaendelea kuimba nyimbo zake zilizopachikwa jina “Abbah.”
RELATED: Jay Melody – Therapy Full Album
Abbah alisema, “Wakinyamaza, nitaleta sauti mpya waendelee kujifunza. Hatuwezi kujivunia Amapiano pekee, tujaribu pia midundo mingine.”
Akizungumza kwenye kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, S2kizzy alisema Tanzania ina watayarishaji wengine wazuri ambao wamefanya kazi nzuri na kufikia mafanikio makubwa, kama vile Nahreel na T Touch. “Baada ya P Funk Majani, ni mimi,” alisema S2kizzy, akiongeza kuwa hakuna mtayarishaji mwingine aliyewahi kutengeneza nyimbo hit 50.
RELATED: Marioo – Hakuna Matata (Prod. S2kizzy)
Je, nani ni producer mkali kwako kati ya hawa wawili?