ENTERTAINMENT

Sukari ya Zuchu yafika 100M – Diamond Ampongeza

Diamond Ampongeza Zuchu, Video Ya "SUKARI" Views 100M

Nyota wa Muziki Afrika, Simba 🦁 @diamondplatnumz, ametuma salamu za pongezi kwa msanii wake @officialzuchu kwa kufikia hatua kubwa ya kuwa msanii wa kwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki kuvuta zaidi ya milioni 100 za kutazamwa kwenye video yake bila kushirikisha msanii mwingine yeyote.

RELATED: Mzeewa Mjegeje Amefariki Dunia leo Alfajiri

“Ukiangalia kwa juu inaonekana kama jambo rahisi, lakini ukianza kujaribu ndipo unatambua ugumu wake!! SUKARI: Imeimbwa na MSANII WA KIKE pekee, 100% Wimbo kwa Kiswahili, Hakuna Ushirikiano! Watazamaji Milioni 100! Ni fahari kubwa kwa @wcb_wasafi, Sekta ya Muziki na Taifa” – Alisema Diamond Platnumz.

Zuchu amefanikiwa kuvutia idadi hiyo ya watazamaji kupitia wimbo wake wa “Sukari” uliotolewa miaka mitatu (3) iliyopita chini ya lebo ya @wcb_wasafi, ambao sasa unakuwa wimbo wake wenye watazamaji wengi zaidi.

Sukari ya Zuchu yafika 100M – Diamond Ampongeza

Also check more tracks from Zuchu;

Leave a Comment