Sakata la Baba Levo na familia yake limechukua sura mpya na limekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii. Mke wake, Salma Mdoli maarufu kama Mama Ruby, amelalamika mtandaoni kwamba Asmah amekuwa akimroga Baba Levo ili aachane na Mama Ruby na awe na Asmah pekee.
- RELATED: Diamond Platnumz Ft Khadija Kopa – Nasema Nawe
- RELATED: Rayvanny Ft Diamond Platnumz – Vumbi (Prod. S2kizzy)
- RELATED: Diamond Platnumz – Jeje (Prod. Kel P)
- RELATED: Zuchu Ft Mbosso – Ashua
Mama Ruby ameeleza kuwa Asmah alitaka hata kuharibu ujauzito wake kwa kutumia mbinu za kishirikina. Haya yote yamekujulikana zaidi baada ya Baba Levo kurejea kutoka safari yake ya kikazi nchini China, ambapo alirejea na zawadi kwa ajili ya Mama Ruby na Asmah. Hili lilimkera Mama Ruby, na akaamua kumkemea Asmah.
Kwa upande wake, Baba Levo alitoa ufafanuzi kuhusu suala hili mtandaoni. Alisema kwamba uhusiano wake na Asmah ulianza baada ya Mama Ruby kumpeleka polisi na ustawi wa jamii, kumwacha na watoto, na hivyo kuhitaji msaada wa mtu wa kuwalea watoto. Asmah alikuja kumsaidia katika hali hii, na uhusiano wao ukakua.
Baada ya Baba Levo na Mama Ruby kurudiana na kuomba msamaha hadharani, Baba Levo alimweleza Mama Ruby kwamba Asmah amekuwa msaada mkubwa kwake na hawezi kuachana naye. Alisema atahitaji Mama Ruby kuonyesha ukomavu wa kitabia na kuthibitisha kwamba hataondoka tena ili kurudisha imani.
Baba Levo ameonyesha kukerwa kwake na Mama Ruby kwa kuyaanika masuala ya familia yao mtandaoni, akisema kuwa hili linahatarisha kazi yake na sifa yake kama kioo cha jamii. Ameeleza kuwa kwa sasa hawezi kurudi nyumbani, na atakaa na Asmah mpaka hali itakapotulia na Mama Ruby akijirekebisha. Sakata hili linaonekana kuwa na athari kubwa si tu kwa familia yao, bali pia kwa sifa za Baba Levo kama mtu maarufu katika jamii.