ENTERTAINMENT

Haji Manara avujisha Video Ya Dulla Makabali baada Dulla kuvujisha Chat

Haji Manara avujisha Video Ya Dulla Makabali baada Dulla kuvujisha Chat

Sakata kati ya Dulla Makabila, Haji Manara, na Zaylissa limeendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii. Hali hii imechochewa na hatua ya Dulla Makabila kuachia wimbo unaomponda Zaylissa, aliyekuwa mke wake, hasa baada ya Zaylissa kuposwa na Haji Manara na kupewa zawadi ya gari katika sherehe yao ya “The Royal Birthday.”

Wimbo huu umepata umaarufu mkubwa, ukiwa nambari moja katika chati za muziki zinazotrend nchini Tanzania. Kufuatia uachiaji wa wimbo huo, Haji Manara alionyesha kutofurahishwa kwake na alimfuata Dulla kwenye DM ya Instagram, akitangaza vita dhidi yake kwa madai ya kumdhalilisha.

Katika hatua ya kujibu, Haji Manara ametoa video inayomuonesha Zaylissa na Dulla, ambapo Dulla anasikika akimlilia Zaylissa na kuomba warudiane, akidai bado anampenda kwa dhati.

Kwa upande wake, Dulla ameibuka na hoja mpya, akimwambia Haji kuwa kumbukumbu zake zinamwambia kuwa Haji alikuwa akimuunga mkono kwa kupost nyimbo zake kwenye Instagram. Lakini, kwa wimbo aliotoa jana, ambao umefikia nafasi ya kwanza kwenye trending bila ya Haji kuupost, Dulla anashangaa kama Haji hajaupenda na kama kuna mambo ya kurekebisha, atamjulisha kwani bado yupo studio na hatatoa video mpaka Haji amuunge mkono.

Also, check out more songs from Dulla Makabila;

Leave a Comment