Katika kile kinachoonekana kama mabadiliko ya ghafla, msanii maarufu wa Bongo Flava, Diamond Platnumz, amebadili msimamo wake juu ya hali yake ya kimapenzi. Mapema leo, Diamond alitangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa yeye ni SINGLE, akisisitiza kuwa hana mahusiano na mwanamke yeyote kwa sasa.
- RELATED: Diamond Platnumz Ft Khadija Kopa – Nasema Nawe
- RELATED: Rayvanny Ft Diamond Platnumz – Vumbi (Prod. S2kizzy)
- RELATED: Diamond Platnumz – Jeje (Prod. Kel P)
- RELATED: Zuchu Ft Mbosso – Ashua
Alisema, “Ningependa niwatangazie rasmi kuwa I AM SINGLE, si date wala sina mahusiano na mwanamke yoyote… hivyo nisiwekewe mwanamke yoyote kama mwanamke wangu, itapotokea ku date ama kuwa na mahusiano nitawajuza ama kuwatambulisha as i always do!”
Hata hivyo, katika muda mfupi tu baada ya tangazo hilo, Diamond ameibuka tena na kauli inayokinzana na ile ya awali. Amesema kuwa suala la kuwa SINGLE limeonekana kuwa gumu kuliko alivyotarajia na sasa anaendelea kufurahia maisha. Amechagua kutumia muda wake kwenye Kisiwa na Kitongoji cha Karafuu, akionekana kuwa na furaha na amani.
Diamond aliongeza, “Na wote Mliokua mnashadadia poleni sana, siku nyingine acheni papara, mjifunze kuskilizia hata kidogo! Watu hawaachani hivyo”. Kauli hii imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku mashabiki na wafuatiliaji wakibaki kuchanganyikiwa na mabadiliko haya ya ghafla katika maisha ya kimapenzi ya msanii huyo maarufu.
