ENTERTAINMENT

Mtoto wa Nabii GeorDavie, Director Nisher Afariki Dunia

Mtoto wa Nabii GeorDavie, Director Nisher Afariki Dunia

Director Maarufu wa Bongofleva na Mtoto wa Nabii GeorDavie, Nisher, Afariki Dunia

Nic Davie, maarufu kama Nisher, mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako, Dr. GeorDavie, na director mashuhuri wa video za Wasanii wa Bongofleva, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 12 Desemba 2023 saa nane na dakika tisa.

Kifo cha Nisher kimepokelewa kwa masikitiko makubwa, hususan kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki wa Bongofleva, ambapo aliweza kuongoza video kadhaa maarufu kama vile “Kijukuu” ya Young Dee, na “Nje Ya Box” ya Niki Wa Pili, Gnako & Joh Makini. Familia ya Dr. GeorDavie imethibitisha tukio hili la kuhuzunisha na imeeleza kuwa msiba utafanyika katika Nyumba ya Matamko, Kisongo, Jijini Arusha. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi na taratibu nyingine zitatolewa baadaye.

Habari za kifo chake zilitangazwa pia kupitia ukurasa wa Instagram wa baba yake mzazi, Nabii Geodavie. Kupoteza kwa Nisher ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki na video nchini, ambapo alikuwa amejijengea sifa na heshima kubwa kutokana na kazi zake bora na za kipekee.

Leave a Comment