MAKALA

Historia fupi ya maisha ya Alikiba

Historia fupi ya maisha ya Alikiba

Ali Salehe Kiba (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ali Kiba; pia: King Kiba; alizaliwa mkoani Iringa 26 Novemba 1986) ni mwanamuziki wa Tanzania, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo chini ya lebo yake King’s Music records na lebo aliyokuwa akiifanyia kazi Rockstar4000, ambayo alikuwa miongoni mwa wamiliki wa lebo hiyo.

RELATED: Alikiba – Mshumaa (Prod. Mocco)

Ana vipaji vilivyo tofauti na wasanii wenzake, hivyo amejikita sehemu nyingine kwa kusajiliwa na Coastal Union kucheza mpira wa miguu kwa msimu wa 2018/2019 wa Vodacom Premier League.

Ali Kiba alizaliwa na wazazi wake Saleh Omari na Tombwe Njere. Ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne kwenye familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba ambaye pia ni mwanamuziki, Zabib Kiba (dada yake) na Abuu Kiba (mdogo wao wa kiume wa mwisho).

Mwaka 2011, Ali Kiba alichaguliwa kama msanii wa kwanza wa Afrika Mashariki – Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwa mwaka 2015 ameshinda tuzo tano za Kilimanjaro Awards.

RELATED: Alikiba – Utu (Prod. Yogo Beats)

Tarehe 20 Mei 2016, kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na muziki “Sony Music Entertainment” ilitangaza kumsainisha mkataba wa kufanya kazi na Ali Kiba.

Also, check more tracks from Alikiba;

Leave a Comment