ENTERTAINMENT

Diamond Platnumz – video ya Waah yafikisha Watazamaji Milioni 100

Diamond Platnumz - video ya Waah yafikisha Watazamaji Milioni 100

Msanii SIMBA Diamond Platnumz amezidi kuweka historia kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya video yake ya “Waah” kuweza kutazamwa mara Milioni 100 kwenye mtandao wa YouTube.

RELATED: Diamond Platnumz Ft Koffi Olomide – Waah! (Prod. Lizer)

Video hio haijavunja rekodi ya ngoma ya ‘Yope Remix’ ambayo ilifikisha watazamaji Milioni 100 ndani ya miezi 10 pekee.

Video ya ‘Waah’ inakuwa ni video ya tatu kutoka kwa Diamond Platnumz kufikisha watazamaji Milioni 100 kwani video nyingine ni pamoja na ‘Yope Remix’ ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 178 pamoja na ‘Inama’ ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 104 kwenye mtandao wa YouTube.

Aidha, kutoka kwenye video ya ‘Waah’, Diamond Platnumz aliweza kuweka rekodi tofauti tofauti ikiwemo ‘Waah’ kutazamwa mara laki moja ndani ya saa moja, rekodi ambayo Harmonize alikuja kuivunja kupitia video yake ya ‘Attitude’ ambayo ilitazamwa mara laki moja ndani ya dakika 44 tu.

Pia, ‘Waah’ iliweza kuweka rekodi mpya kwenye muziki wa Afrika baada ya kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 8 tu na hivyo kupiku rekodi ya Davido ambaye video yake ya ‘Fem’ ilitazamwa mara Milioni 1 ndani ya saa 9.

RELATED: Innoss’B Ft Diamond Platnumz – Yope Remix

Ikumbukwe pia kuwa Diamond Platnumz ndie msanii anayeongoza kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi kusini mwa jangwa la sahara akiwa na wafuatiliaji Milioni 6 kwenye akaunti yake hiyo huku akiwa ameshatazamwa mara Bilioni 1.6 kwenye mtandao wa YouTube.

Source: Mdundo

Also, check more tracks from Diamond Platnumz;

Leave a Comment