Kupitia account yake ya Instagram, Star wa muziki wa kizazi kipya anayetamba kwa wimbo wake mpya “Jeje” Diamond Platnumz ametangaza rasmi kwamba shida za watu wa jamii yake ni zake.
Diamond Platnumz anunua gari jipya โRolls Royce Dawnโ million 899
Katika post hiyo Diamond Platnumz amefunguka kuhusu janga la Corona ambalo linaikumba dunia kwa sasa na yuko tayari kulipia kodi za nyumba ya miezi mitatu kwa familia 500.
Alisema japo kuwa na yeye ni miongoni ya walioathirika na janga hilo lakini bado yuko tayari kusaidia jamii yake katika kile kidogo ambacho Mungu amempa.
Utarituba wa namna ya kupata misaada hiyo utatolewa rasmi jumatatu hii..
Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biasharaโฆ. nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetuโฆ
Ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Coronaโฆ
Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu piaโฆ.
Wema Sepetu akerwa kuitwa EX wa Diamond Platnumz
Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumbaโฆ.?? HiliNaloLitapita #ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona – Aliandika Diamond Platnumz
