Aina za maneno – Kiswahili
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wazimebainisha. Aina hizo ni nomino (N), viwakilishi (W), vitenzi (T), vivumishi (V), vielezi (E), viunganishi (U), vihusishi (H), vihisishi (I).