LIFESTYLE

Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi

Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi
Amber Lulu -Picha haihusiani na makala
Njia 6 za kumjua msichana ambaye hakupendi

1. Anakataa kukupa namba mara ya kwanza
Ikiwa msichana hataki kukupa namba yake ya simu unapomuomba mara ya kwanza, jua ya kwamba hakutaki. Ikiwa atakupa, itachukua muda kufanya hivyo, jua kuwa hataki mambo yako, hivyo ni bora kukoma mapema kwa sababu mtasumbuana bure tu.

RELATED: Njia muhimu 6 za kurefusha nywele za kiafrika hasa wanawake

2. Amekupa namba isiyo yake
Msichana akifanya hivi huhitaji kungoja sana kujua kuwa hapendezwi nawe. Kushinda ukimfuata itakuumiza bure tu kwani simu zako zitakuwa zikichuliwa na mtu mwingine. Huenda akalaumu mfumo mbaya ya mawasiliano.

3. Hapokei simu unapompigia
Unangoja nini kujua hakutaki? Ikiwa msichana atachukua simu mara moja unapopiga, jua ya kuwa anakupenda na ni ishara kuwa mtakuwa marafiki. Lakini akichukua muda kujibu, kimbia

4. Hakutembelei
Ikiwa hatembei kwako, basi ni ishara kwamba hataki kukuona. Hakuna haja ya kumfuatafuata.

5. Ukisikia marafiki wake wakicheka unapompigia simu
Ikiwa atafanya hivyo, hiyo ni tahadhari, huenda anakudharau. Utangoja mpaka akuvunje moyo? Endelea na maisha yake, utapata mwingine anayekupenda.

6. Anapotumia pesa zako ovyo ovyo “Baadhi ya wanawake sio wema”. 
Licha ya kuamua kutokuwa na uhusiano wowote nao, wanapenda tu kutumia wanaume vibaya kwa kuwasaidia kuharibu pesa zao walizofanyia kazi kwa bidii.

RELATED: Mwanamke akikupenda utaona vitu hivi 10

Ikiwa hakupendi, ataandamana na marafiki wake wote unapomualika na kukufanya kutumia pesa zaidi ya ulivyokuwa umepanga.

Also, check more tracks from Alikiba;

Leave a Comment