Wednesday, December 4, 2019

Faida 6 za kufanya mapenzi katika mahusiano

Kufanya mapenzi ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Huwakutanisha na kuwaweka pamoja wewe na mpenzi wako. Mapenzi hulifanya penzi lenu kuwa hai.

Kufanya mapenzi ni kichocheo muhimu cha kuamsha hisia zenu za kimahaba. Hii ni mada kuu inayopendwa na huongelewa sana na wanaume pamoja na wanawake.

Ni kitu ambacho kila mtu hukifikiria hata kama hawako katika hali ya mapenzi. Kwa kweli ni muhimu tu kama uaminifu na mawasiliano.

Kujamiiana hutofautiana baina ya mwanaume na mwanamke. Ni aina mojawapo maarufu ya kukupa furaha na kukuondolea mawazo. Pia huwaweka karibu wewe na mpenzi wako.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwa nini kufanya mapenzi ni muhimu katika mahusiano.

Hukuza urafiki baina yenu na kuimarisha mahusiano.
Kuwa na mpenzi ambaye ni rafiki yako ni jambo zuri sana katika mahusiano. Kuwa katika mahusiano pasipo kufanya mapenzi na mwenza wako ni kama tu kuwa na rafiki yako. Mahusiano hujawa na uchu, wapenzi hutaka furaha na kuridhika. hivyo kufanya mapenzi na mwenza wako huchochea hisia nzito baina yenu, huburudisha na kuyafanya mahusiano kuwa bora.

Huondoa mawazo
kufanya mapenzi husaidia kuondoa mawazo. ufanyapo mapenzi homoni zinazokupa furaha hutengenezwa kwa wingi wilini. Kumbuka unapokuwa na furaha ndivyo unavyoweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Huyafanya mahusiano kuwa hai.
Kujamiiana ni kitu ambacho unaweza kufanya ili kujifurahisha wewe pamoja na mwenzi wako. Hukuza urafiki na kuwa na hakika, vile vile huwafanya mujione kuwa kila mmoja anahitajika na mwenzake.

Kufanya mapenzi ni njia nzuri ya kuwasiliana, huwafnya kupendana zaidi na kuuona umuhimu wa kila mmoja katika maisha yenu ya mahusiano.

Hukufanya uwe na usingizi mwanana.
kufanya mapenzi hukufanya ulale usingizi mzuri. Siyo kwa sababu ya uchovu wa shughuli nzito mliyoifanya. Unapomaliza kufanya mapenzi kemikali iitwayo ‘oxytocin’ huachiwa na mwili. Hii hukufanya kulala usingizi mzuri na wa raha.

Hukupa furaha.
Watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na furaha zaidi ya wale wanaofanya mara chache au wasiofanya kabisa. Vile vile hukuongezea kujiamini na kuwa na mtazamo chanya katika maisha.

Humpa furaha mwenza wako.
Kufanya mapenzi huwafanya wanaume wanapokuwa na msongo wa mawazo, kujisikia furaha. Kama uko kwenye mahusiano na huwa hamfanyi mapenzi mara kwa mara, kuna hatari kuwa mwenza wako hapati furahaa 100%. Hivyo kama hamtofanya mapenzi, kuna uwezekano wa yeye kwenda kutafuta mtu mwingine wa kufanya nae mapenzi. hivyo ili kumfurahisha ni vyema muwe mnafanya mapenzi mara kwa mara.