MAKALA

Dalili za kwanza za mimba changa – wiki moja na kuendelea

Dalili za kwanza za mimba changa - wiki moja na kuendelea
Dalili za kwanza za mimba changa – wiki moja na kuendelea

MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

RELATED: Siku za kupata au kushika mimba (Jifunze hapa)

Maumivu kwenye matiti:
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini:
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kutokwa damu bila kutegemea:
“Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.

“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi”

Chuchu kuwa nyeusi:
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”

RELATED: Siri 6 za wanawake ambazo kamwe hawawezi kukuambia. Zisome hapa

Kichefuchefu:
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba:
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Dalili za kwanza za mimba changa – wiki moja na kuendelea

Kwenda haja ndogo mara kwa mara:
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali:
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebish a na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.

Kuwa na hasira
“Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”

Kuongezeka kwa joto mwilini:
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.

 
 

7 Comments

  • Matiti yamejaa miguu imejaa na mdomo hauna ladha ila tareh 2 nimepata period siku 4 na mwanzo nilikuwa na dalili za mimba naomba ushaur itakuwepo mimba au ntakuwa sina nimepima kwenye kipimo cha mkojo sina ila dalili zote ninazo mwilin

  • Kuna uhusiano wowote Kati ya mtoto mwenye three years akiugua inakuwa ni dalili ya mwanamke kuwa na mimba na kwamba mtoto anaugua kwa sababu ya joto la mwili wa mama ??

  • Sijapata siku zangu miezi miwili na nikipima ujauzito Sina ila dalili zote za mimba ninazo je ni tatizo au ujauzito??

  • Mim ikifk mida ya asbh nahis kuchoka nakuna muda nikiwa kazin akija mtej Kam nimelala napatwa na hasira na pia tumbo Kam limevimba alafu chuchu nikizishika zinauma

Leave a Comment