MAKALA

Dalili za mimba ya wiki moja

Dalili za mimba ya wiki moja

Dalili za mimba ya wiki moja: Hutokea mara nyingi kina mama na wasichana kuwa na kipindi cha msongo wa mawazo pale wanapokosa siku zao na hasa kama hawakutumia njia ya uzazi wa mpango au kinga nyingine ya kushika mimba.

RELATED: Kitakachompata mwanamke akiacha kufanya mapenzi

Kukosa siku zako sio dalili pekee ya kushika mimba, bali kuna dalili zingine utalazoziona. Kuna sababu nyingine nyingi zinazoweza kukufanya ukose siku zako, hivyo soma dalili za mimba ili ikusaidie kupata uhakika.

1. Mabadiliko katika siku zako. Hii kitaalamu tunaita spotting. 

Unaweza kushika mimba ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza kwenye kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa kwenye ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo amabazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango na siku za damu hubadilika.

2. Kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa. 

Hii inasababishwa na ongezeko la homoni za istrogen pale unapokuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

3. Kichefuchefu na kutapika. 

Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapoToka kulala. Hii ni kwa sababu ya homoni ya ‘projestroni’ ambayo husababisha kupungua nguvu kwa misuli ya mrija wa chakula au koromeo.

RELATED: Ukipata mwanamke mwenye sifa hizi 16 usimwache

4. Uchovu usiokuwa na usingizi usiokuwa na sababu. 

Hii hutokea kwa sababu ya ongezeko la homoni ya ‘projestroni’ na mama utajikuta unasinzia mara kwa mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba ila hata kipindi cha mwisho wa mimba hujisikia uchovu.

5. Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. 

Hasa kama unapata mimba kwa mara ya kwanza, utachukia harufu za vyukula na vinywaji mabalimbali. Wakati mwingine hata harufu za watu walio karibu nawe zinaweza kukukera.

6. Kujaa gesi tumboni. 

Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi hasa sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinazokufanya kijisikia tumbo kujaa.

7. Kukojoa mara kwa mara. 

Hii kwanza hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa rishe ya kutosha kwako na kwa kiumbe tumboni. Ukiwa na damu nyingi pia utakojoa sana za kikemia mwilini. Pili utajisikia kwenda haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitakapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

RELATED: Mambo 15 mwanamke huangalia kabla ya kukupenda

8. Kuongezeka kwa joto la mwili. 

Kwa kina mama ambao hupima joto lao kama njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfurulizo.

9. Kutoona siku sako kabisa. 

Kwa wale ambao siku zao hazibadiliki na huenda vizuri yawezekana kugundua pale wanapokose siku nap engine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona kawaida ila kama ameshika mimba taona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu na kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

10. Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. 

Famasi nyingi huuza vipimo ambavyo ikikichovya kwenye mjojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo.

Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani hata kazini. Kipimo hiki ukisha kichovya kwenye mkoja kama katatsi inavyoelekea utaona mistali baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini.

RELATED: Jinsi ya kutumia sekunde tatu kumtongoza mwanamke

Ikitokea mistari miwili basi unaweza kuwa na mimba na ukitokea mmoja utakuwa huna mimba. Kilingana na kiwango cha homoni mwilini, kuna kina mama hakionyeshi majibu mpaka upitishe wiki moja bila kuona siku zako.

Pamoja na dalili hapo juu, unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari.

Dalili za mimba ya wiki moja

5 Comments

Leave a Comment