MAKALA

Dalili za mimba changa (Mimba ya siku tatu)

Utagunduaje kama una mimba changa? Soma hapa

Katika siku za awali za ujauzito, mwanamke anaweza kupitia mabadiliko kadha wa kadha mwilini mwake. Mojawapo ya dalili za kwanza ni kuvimba kwa matiti na maumivu au muwasho kwenye chuchu. Ni kawaida pia kwa baadhi ya wanawake kuona ongezeko la mavuzi na kubadilika kwa rangi ya chuchu zao kuwa nyeusi.

Karibu nusu ya wanawake wajawazito hupata maumivu ya tumbo na wakati mwingine hali ya kutapika. Mara nyingi, wanawake hujikuta wakihisi haja ya kukojoa mara kwa mara na wengine hupitia uchovu mkubwa na kizunguzungu, hususan katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito.

Mabadiliko katika upendeleo wa vyakula ni jambo lingine linaloweza kutokea, ambapo wanawake wengine hupata hamu ya kula vyakula fulani au kuchukia vyakula walivyovizoea. Ili kuthibitisha ujauzito, ni muhimu kwa mwanamke kufanya vipimo vya mkojo katika kliniki au hospitali iwapo anahisi kuwa na mimba.

Leave a Comment